Вход на сайт

Просмотр новости

Найдите то, что Вас интересует

Keiko aweka historia Peru, aahidi kujenga gereza kubwa

Дата публикации: 29-07-2026 08:29:09

Keiko Fujimori ameapishwa rasmi kuwa rais wa kwanza mwanamke katika historia ya Peru, akifungua ukurasa mpya wa uongozi katika taifa ambalo limekumbwa na misukosuko ya kisiasa kwa karibu muongo mmoja.

Основное содержимое страницы с новостью.

Muktasari:
  • Keiko Fujimori ameapishwa kuwa rais wa kwanza mwanamke wa Peru, akiahidi kurejesha utulivu wa kisiasa, kuimarisha uchumi na usalama, pamoja na kujenga gereza kubwa litakaloiga mfumo wa CECOT wa El Salvador.

Lima, Peru. Keiko Fujimori ameapishwa rasmi kuwa rais wa kwanza mwanamke katika historia ya Peru, akifungua ukurasa mpya wa uongozi katika taifa ambalo limekumbwa na misukosuko ya kisiasa kwa karibu muongo mmoja.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 51 na Mwenyekiti wa Chama cha Fuerza Popular anaingia madarakani baada ya kushinda uchaguzi Juni mwaka huu, ushindi unaoashiria kurejea kwa familia ya Fujimori katika uongozi wa Peru baada ya miaka kadhaa ya kushindwa kufanikiwa katika harakati za kisiasa.

Fujimori aliapishwa jana Jumanne, Julai 28, mbele ya Bunge la Peru, akiapa kutekeleza majukumu yake kwa uaminifu na kuiongoza nchi kuelekea utulivu baada ya miaka ya misukosuko ya kisiasa.

Katika kampeni zake, aliahidi kutumia ‘mkono wa chuma’ kukabiliana na ongezeko la uhalifu, ukiwamo mtandao wa magenge ya ndani na ya kimataifa yanayohusishwa na mauaji ya kulipwa na vitendo vya ujambazi.

Katika kutekeleza mkakati huo, ameahidi kujenga gereza kubwa litakaloiga mfumo wa gereza la CECOT nchini El Salvador (CECOT au kwa kirefu ‘Centro de Confinamiento del Terrorismo’ ni gereza lenye ulinzi mkali sana chini ya utawala wa Rais Nayib Bukele. Lilitengwa kuwahifadhi wanachama wa magenge hatari na wahalifu wa ugaidi, hususan magenge ya MS-13 na Barrio 18, na lina uwezo wa kuhifadhi hadi wafungwa 40,000).

Katika kuimarisha utulivu na haki rais huyo amesema kuwa atatumia majaji wasiojulikana kusikiliza kesi za uhalifu mkubwa, kuwafukuza wahamiaji wasiokuwa na vibali na kuwataka wafungwa kufanya kazi ili kujipatia chakula.

Akihutubia baada ya kuapishwa, Fujimori alisema serikali yake itaweka kipaumbele katika kurejesha usalama, imani ya wananchi kwa taasisi za dola na kuimarisha uchumi. Kwa mujibu wa Deutsche Welle (DW), Reuters na AP, serikali hiyo itafanya kazi kwa karibu na washirika wa kimataifa, akieleza kuwa kuna fursa kubwa ya kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kidiplomasia kati ya Peru na Marekani.

Ushindi wake ulitokana na kumshinda mgombea wa mrengo wa kushoto, Roberto Sánchez, kwa tofauti ya kura zisizofikia 50,000 katika duru ya pili ya uchaguzi uliofanyika Juni. Kabla ya ushindi huo, Fujimori alikuwa amegombea urais mara tatu bila mafanikio.

Kuapishwa kwake kunamfanya kuwa rais wa 10 wa Peru ndani ya kipindi cha miaka 10 tangu mwaka 2016, hali inayoonyesha kuyumba kwa siasa za taifa hilo ambako marais kadhaa waliondolewa madarakani, walijiuzulu au walishindwa kumaliza mihula yao.

Fujimori ni binti wa rais wa zamani wa Peru, Alberto Fujimori, aliyeiongoza nchi hiyo kuanzia mwaka 1990 hadi 2000. Utawala wake ulisifiwa kwa kudhibiti mfumuko wa bei na kupambana na waasi wa Shining Path, lakini pia ulikosolewa vikali kwa ukiukwaji wa haki za binadamu na tuhuma za ufisadi zilizomfikisha gerezani.

Схожие новости

#Наименование новостиТональностьИнформативностьДата публикации
1Keiko Fujimori será presidenta5701-07-2026
2Кейко Фухимори вступает в должность президента Перу. Каким был ее путь013.5328-07-2026
3Кейко Фухимори стала президентом Перу0730-06-2026
4Fujimori triunfa en los comicios presidenciales de Perú0503-07-2026
5Conservative candidate Keiko Fujimori wins Peru’s presidential election in a runoff0503-07-2026
6Президентские выборы в Перу выиграла Кейко Фухимори0530-06-2026
7Fujimori promete trabajar para terminar con la "desigualdad" y el "enfrentamiento" en Perú0515-07-2026
8Кейко Фухимори официально победила на выборах президента Перу0704-07-2026
9Keiko Fujimori se prepara para gobernar Perú: cuándo será proclamada presidenta electa0525-06-2026
10Huyu hapa Miss Tanzania wa kwanza wa mwaka 1967017.7820-07-2026

Классификация: Информация. Схожих патентов: 0. Схожих новостей: 10. Тональность: 0. Информативность: 7.09. Источник: www.mwananchi.co.tz.