Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Alex Malasusa, leo Julai 29, 2026 anatarajiwa kuongoza ibada ya kuaga mwili wa Mchungaji Silvanus Msuya (44) katika Usharika wa Boko, Dayosisi ya Pwani na Mashariki, jijini Dar es Salaam, ambapo mamia ya waumini wa kanisa hilo watapata wasaa wa kushiriki ibada hiyo na kuaga mwili.
Moshi. Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Alex Malasusa, leo Julai 29, 2026 anatarajiwa kuongoza ibada ya kuaga mwili wa Mchungaji Silvanus Msuya (44) katika Usharika wa Boko, Dayosisi ya Pwani na Mashariki, jijini Dar es Salaam, ambapo mamia ya waumini wa kanisa hilo watapata wasaa wa kushiriki ibada hiyo na kuaga mwili.
Mchungaji Silvanus Msuya alifariki dunia Julai 26, 2026 katika Hospitali ya Rabininsia, jijini Dar es Salaam, alipokuwa amelazwa akisumbuliwa na nimonia kali. Ameacha mke na watoto watatu.
Novemba 3, 2024, Mchungaji Silvanus alibarikiwa kuwa mchungaji wa Dayosisi ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro, na amekuwa mchungaji kiongozi wa Usharika wa Spillway, Jimbo la Tambarare, mchungaji mwenza wa Usharika wa Kanisa Kuu Mwanga na Mratibu wa Habari na Mawasiliano wa Dayosisi ya Mwanga.
Akizungumza na Mwananchi, kaka wa marehemu, Elisa Msuya, amesema ibada ya kuaga mwili wa mpendwa wao itaanza saa mbili asubuhi leo Julai 29, 2026 katika Usharika wa Boko na kumalizika saa sita asubuhi.
Amesema baada ya taratibu zote za ibada na kuaga mwili wataanza safari kuelekea Wilaya ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro, ambapo mwili wa Mchungaji Silvanus utapumzishwa nyumbani kwao katika Kijiji cha Shighatini kwa ajili ya taratibu za maziko.
Amesema kesho Julai 30, mwili wa mchungaji huyo utapelekwa katika Kanisa Kuu la KKKT Mwanga kwa ajili ya ibada ya mazishi, ambapo amesema taratibu zote za kiibada zitakapokamilika mwili utapelekwa katika Kanisa la Shighatini, ambapo ndipo mwili huo utakapozikwa.
"Mwili utakapofika Mwanga leo utapumzishwa Kijiji cha Shighatini, ambapo kesho asubuhi kuanzia saa 2 hadi saa 4 asubuhi kutakuwa na shughuli ya kuaga. Baada ya hapo kutakuwa na salamu mbalimbali na kuanzia saa 6 mchana kutakuwa na ibada ya mazishi, na baada ya hapo mwili wake utazikwa katika Kanisa la Shighatini," amesema kaka wa marehemu.
| # | Наименование новости | Тональность | Информативность | Дата публикации |
|---|---|---|---|---|
| 1 | Masaju anavyoibua matarajio mhimili wa Mahakama | 0 | 10 | 28-07-2026 |
| 2 | В Духовной столице Сибири молитвенно почтили память святителя Иоанна, митрополита Тобольского | 5 | 7 | 24-06-2026 |
| 3 | Проповідь Блаженнішого Святослава до 100-ліття Мукачівської чудотворної ікони Богородиці | 5 | 5 | 24-06-2026 |
| 4 | Проповідь Блаженнішого Святослава у Понеділок Святого Духа | 0 | 0 | 01-06-2026 |
| 5 | Божественна Літургія з Патріаршого собору УГКЦ | 5 | 3 | 21-06-2026 |
| 6 | La homilía de 30 de julio de 2025 | 0 | 0 | 30-07-2025 |
| 7 | El Cascabel, 27 de julio de 2026 | 0 | 31.84 | 27-07-2026 |
| 8 | Pride of YLLSS: Illuminating Life Through Rectify Mind Cultivate Person | 0 | 24.29 | 22-05-2026 |
| 9 | Слово Святейшего Патриарха Кирилла на встрече с преподавателями богословских курсов для монашествующих Валаамского монастыря | 0 | 5 | 10-07-2026 |
| 10 | El Cascabel, 7 de julio de 2026 | 0 | 31.84 | 09-07-2026 |