Soma zaidi hapa...
Uteuzi wa Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, George Masaju, umeibua matarajio mapya kuhusu nafasi ya Mahakama katika kuimarisha utawala wa sheria na utoaji wa haki nchini.
Kauli zake za hivi karibuni zimeonyesha msimamo unaosisitiza kuwa hakuna mtu, taasisi wala mhimili wa dola ulio juu ya sheria. Huo ni ujumbe wenye uzito mkubwa kwa mustakabali wa haki, utawala bora na maendeleo ya taifa.
Katika hotuba yake, Jaji Mkuu Masaju amesisitiza kuwa jukumu la Mahakama ni kutenda haki bila hofu, upendeleo au chuki. Amesisitiza pia kwamba hata yeye binafsi hayuko juu ya sheria, bali ameapa kuisimamia Katiba na sheria za nchi kwa uadilifu. Kauli hiyo inadhihirisha dhamira ya kulinda misingi ya uhuru wa Mahakama na kuhakikisha haki inatolewa kwa mujibu wa sheria.
Msimamo huo unastahili kuungwa mkono kwa sababu Mahakama ndiyo nguzo ya mwisho ya wananchi wanapotafuta haki.
Imani ya wananchi katika mfumo wa utoaji haki hujengwa pale wanapoona maamuzi ya Mahakama yanaheshimiwa na kutekelezwa na kila mtu bila kujali cheo au mamlaka aliyonayo.
Jaji Mkuu pia amekemea tabia ya baadhi ya viongozi na taasisi za umma kupuuza au kuchelewesha utekelezaji wa maamuzi ya Mahakama. Alisisitiza kuwa mamlaka zinazotolewa na sheria kwa taasisi mbalimbali hazizipi ruhusa ya kuingilia utekelezaji wa amri halali za Mahakama. Kwa mtazamo wake, siasa na utoaji wa haki ni maeneo mawili yanayopaswa kubaki na mipaka yake.
Kauli hizi alizitoa alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa Chama cha Madalali na Wasambaza Nyaraka wa Mahakama Tanzania uliofanyika katika Makao Makuu ya Mahakama jijini Dodoma.
Katika mkutano huo alikumbusha pia wajibu wa kuheshimu Ibara ya 26 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayomtaka kila mwananchi kuheshimu sheria na kushiriki kulinda Katiba ya nchi.
Aidha, Jaji Mkuu alieleza kuwa utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 unategemea kwa kiasi kikubwa uwepo wa utawala bora na mfumo wa haki unaofanya kazi kwa uhuru.
Kwa maoni yake, haiwezekani kujenga utawala bora ikiwa uamuzi wa Mahakama utaendelea kuingiliwa au kupuuzwa na mamlaka nyingine.
Katika hotuba hiyo alinukuliwa akisema: "Hakuna mtu ambaye yuko juu ya sheria na hata mimi Jaji Mkuu siko juu ya sheria. Na kwanza hata mimi kwa kiapo changu na Majaji wote hapa na Mahakimu wote, na hata wasajili tunaapa tunapotekeleza majukumu yetu kuzingatia Katiba, mila na desturi, na sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, bila hofu, upendeleo wala chuki."
Kauli hiyo ni ukumbusho muhimu kwamba utawala wa sheria haupaswi kuwa nadharia bali ni kanuni inayotumika kwa vitendo. Ikiwa Mahakama ndiyo mlinzi wa Katiba, basi uamuzi wake unapaswa kuheshimiwa na kutekelezwa kwa wakati na kwa ukamilifu.
Katika mazingira hayo, hoja ya kuimarisha utekelezaji wa hukumu za Mahakama inapaswa kupewa uzito unaostahili. Kumekuwa na matukio ambayo hukumu hutolewa, lakini utekelezaji wake huchelewa au hukwama kutokana na hatua za baadhi ya taasisi au viongozi. Hali hiyo inaweza kupunguza imani ya wananchi kwa mfumo wa utoaji haki na kuathiri hadhi ya Mahakama.
Kutokana na changamoto hiyo, kuna hoja kwamba Mahakama zinaweza kuendelea kuimarisha mfumo wa utekelezaji wa hukumu kwa kuhakikisha uamuzi wake unaelekeza kwa uwazi wajibu wa kila mhusika, namna ya utekelezaji na muda unaotarajiwa.
Dhamira ya pendekezo hilo ni kufanya hukumu ziwe mahsusi, zinazopimika, zinazowezekana kutekelezwa, zenye uhalisia na zenye muda maalumu wa utekelezaji, dhana inayofafanuliwa kwa kifupi kama Smart. Kwa mtazamo huu, hukumu inapoweka masharti ya utekelezaji ndani ya muda maalumu, inarahisisha uwajibikaji na hupunguza mianya ya kuchelewesha haki.
Aidha, pale ambapo kutakuwa na kukaidi amri halali za Mahakama, sheria zilizopo zinaweza kutumika kuchukua hatua dhidi ya wahusika kwa mujibu wa taratibu za kisheria.
Jaji Mkuu pia aliwakumbusha wanasheria kutumia ipasavyo sheria dhidi ya wanaozuia utekelezaji wa amri za Mahakama au wanaokiuka sheria kwa makusudi.
Alisisitiza kuwa kila anayekiuka sheria anapaswa kuwajibika kwa matendo yake binafsi, bila kujificha nyuma ya taasisi anayoitumikia.
Mbali na masuala ya sheria, Jaji Mkuu alihusisha pia maadili na imani katika utoaji wa haki.
Alisema kuwa haki haiwezi kutolewa kwa uaminifu ikiwa watendaji wataitumia nafasi yao kwa manufaa binafsi au kuwaonea wengine.
Akikumbusha umuhimu wa kumcha Mungu, alinukuu mafundisho yanayosisitiza kwamba kila mtu huvuna alichokipanda na kwamba haki inapaswa kutendwa kwa dhamiri safi.
Kwa ujumla, ujumbe wa Jaji Mkuu Masaju unaonyesha umuhimu wa kulinda heshima ya Mahakama kama msingi wa utawala wa sheria.
Iwapo kila mhimili utatekeleza wajibu wake Tanzania itaendelea kuimarisha utawala bora na kuhakikisha haki inapatikana kwa wote. Kwa sababu katika taifa linaloongozwa na sheria, hakuna aliye juu ya sheria, na hakuna taasisi inayopaswa kuwa juu ya Mahakama inapotekeleza wajibu wake wa kutoa haki.
| # | Наименование новости | Тональность | Информативность | Дата публикации |
|---|---|---|---|---|
| 1 | Kauli 'leo lazima niue mtu' ilivyogeuka hukumu ya kifo | 0 | 10 | 29-07-2026 |
| 2 | Minyukano Inavyozima ndoto za upinzani kushika dola | 0 | 10 | 28-07-2026 |
| 3 | KONA YA MALOTO: Kumwelewa Nchimbi inatakiwa ung’amue alikoficha nukta | 0 | 10 | 28-07-2026 |
| 4 | Sendiga ‘anavyowateka’ wananchi kwa kujifananisha nao | 0 | 10 | 28-07-2026 |
| 5 | Safari ya Kanali Kipingu kunoa kizazi cha wasomi nchini | 0 | 10 | 28-07-2026 |
| 6 | Zanzibar inaandika ukurasa mpya au inarudia historia? | 0 | 10 | 28-07-2026 |
| 7 | Askofu Malasusa kuongoza ibada mazishi ya Mchungaji Silvanus | 0 | 8.54 | 29-07-2026 |
| 8 | Mwalimu auawa akizuia mifugo kupita eneo la shule | 0 | 6.05 | 29-07-2026 |
| 9 | В Сумах вновь произошел взрыв | 0 | 10 | 24-07-2026 |
| 10 | Москалькова предлагает наделить ОНК полномочиями по борьбе с контрафактом в колониях | 0 | 0 | 19-11-2018 |