Вход на сайт

Просмотр новости

Найдите то, что Вас интересует

KONA YA MALOTO: Kumwelewa Nchimbi inatakiwa ung’amue alikoficha nukta

Дата публикации: 28-07-2026 19:08:42

Soma zaidi hapa...

Основное содержимое страницы с новостью.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Emmanuel Nchimbi, amechagua kwenda kwa mtindo wa zamani wa bendi ya African Stars “Twanga Pepeta”, anachofanya ni “kuangusha mojamoja”. Na kila linalomtoka mdomoni linakuwa simulizi ya vyombo vya habari, mitandao ya kijamii mpaka vilinge vya mtaa hadi mtaa.

Moja mpya ni “Katiba Mpya”. Nyuma tayari alishatoa nyingine kadhaa. Katika hotuba yake wakati wa kufungua Mkutano Mkuu wa 15 wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) Ijumaa, Julai 24, 2026, Nchimbi alisema kwa msisitizo, “komaeni tupate Katiba Mpya”. Ulikuwa ujumbe kwa Watanzania hususan wanaharakati. Nchimbi pia alisema matamanio yake ni kuketi na mwanaharakati Maria Sarungi, ambaye amekuwa akimshambulia Rais Samia Suluhu Hassan mitandaoni, kila iitwapo leo.

Kuhusu Katiba, Nchimbi alisema kuwa neno lake moja tu ni hilo, Watanzania hasa wanaharakati wapambane kupata Katiba Mpya. Kisha akataja sifa ya Katiba ambayo yeye anaitamani kwamba iwe ni ile yenye makubaliano ya wadau wote, inayoheshimu haki za wananchi na inayoweza kuliongoza taifa kwa miongo mingi ijayo.

Hoja hapa si “Katiba Mpya”, ni maneno “Pambaneni Tupate Katiba Mpya”, na “Komaeni Tupate Katiba Mpya”. Katiba Mpya ni ahadi ya kwenye Ilani ya CCM. Zaidi, ni ahadi ya Rais Samia. Maneno yoyote yenye kujenga muktadha wa kuelekea kupata Katiba Mpya si tatizo. Ni msimamo wa CCM na Serikali, maana Rais Samia ndiye mkuu wa Serikali. Msimamo wake ndiyo wa Serikali.

Maneno “Komaeni” na “Pambaneni”, ndiyo yanayoibua mgagaziko na kutengeneza viulizo lukuki. Komaeni Tupate Katiba Mpya au Pambaneni, siyo lugha ya Serikali au CCM. Hayo ni matamshi ya wanaharakati na viongozi wa vyama vya upinzani. Sasa kwa nini Nchimbi ameyatumia? Zingatia, Nchimbi ni kiongozi namba mbili kwenye nchi.

Nchimbi anataka kufikisha ujumbe gani? Malengo yake ni yapi? Maswali hayo ili upatie majibu yake, inabidi kwanza ujue mahali alipoficha nukta. Nchimbi anazungumza bila kuweka nukta. Maana yake, sentensi zake hazifiki mwisho.

Anaiacha hadhira njiapanda. Anawashughulisha watu kuutafsiri na kuuelewa ujumbe wake. Bahati mbaya, kila mtu anachagua kuelewa kwa namna yake.

Ona Nchimbi anavyoamua kuchang’anya watu; anasema “komaeni”, halafu anasema Rais Samia ndiye anataka Katiba Mpya. Kisha anatoa kitisho kwamba Katiba Mpya isipopatikana kipindi hiki Rais Samia yupo madarakani, inaweza kuchukua miaka mingine 50 kabla ya kuandikwa Katiba nyingine.

Kokotoa mkanganyiko unaotegenezwa na Nchimbi; Rais Samia ndiye mtoa ahadi. Yeye ndiye Mkuu wa Nchi. Anachokitaka utekelezaji wake hauna kona.

Kila kitu kipo ndani ya mamlaka yake. Wakati huohuo, Nchimbi anatumia sauti ya wapinzani wa kisiasa na wanaharakati kufanikisha kile ambacho kimeshaahidiwa na Rais Samia, pamoja na CCM. Chama kinachoongoza dola.

Ni hapo sasa; ukiwa mwanaharakati, unaona kama Nchimbi anazungumza lugha yako, lakini unahisi kama kuna mtego, kwa hiyo unaogopa kumuunga mkono moja kwa moja.

Ukiwa CCM au kiongozi serikalini, unamwona Nchimbi kama anawaambia Watanzania kuwa Rais Samia ndiye mwenye dhamira njema, hivyo akiondoka yeye, itakula kwao. Unatamani kumpongeza, lakini unakumbuka sauti za kiharakati ndani yake.

Kama Rais Samia anataka Katiba, kwa nini adaiwe? Wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu 2025, Rais Samia aliahidi mchakato wa kupata Katiba Mpya ndani ya siku 100 za mwanzo baada ya kuapishwa.

Siku ya uchaguzi nchi ilikumbwa na dhoruba kubwa. Machafuko yalitokea. Watu zaidi ya 500 walipoteza maisha.

Wengi zaidi walijeruhiwa. Mali za umma ziliharibiwa na kuibwa. Watu binafsi waliporwa na kuharibiwa miliki zao. Miundombinu ilibomolewa na kuchomwa moto kwenye maeneo mbalimbali ya nchi.

Kutokana na mazingira hayo, Novemba 14, 2025, Rais Samia alipokuwa anazindua Bunge la 13, alisema kuwa mchakato wa Katiba ungesubiri ripoti ya matukio ya kadhia Oktoba 29.

Kisha aliunda tume, na ripoti hiyo tayari ilishatoka. Sasa kuna Tume ya Jinai inakanayo na madhila ya Oktoba 29. Kisha yafuate maridhiano, ndipo mchakato wa Katiba uanze.

Rais alipata kusema kuwa haitawezekana kuandika Katiba Mpya nchi ikiwa vipandevipande.

Unapate Katiba ya nchi kila upande ukiwa unavuta kwake. Maridhiano ni kipengele muhimu, ili Katiba ipatikane katika mazingira yenye mwafaka wa kitaifa.

Sasa, kama nchi inasubiri maridhiano kwa mujibu wa miririko ambao Rais Samia anautaka, na ameshautamka, kwa nini Nchimbi anawaambia watu wapambane na wakomalie?

Je, Nchimbi anaamsha watu kupambania Katiba nje ya mtiririko ambao Rais Samia anautaka? Je, “Pambaneni” na “Komaeni”, anaamanisha watu wachangamkie maridhiano ili Katiba ipatikane haraka, vinginevyo hawataipata tena? Hoja yake ni kwa masilahi ya nani? Yake binafsi sasa au kesho anayoilenga? Anaipenda na kuitakia mema nchi? Anafanya hivyo kumtafsiri Rais Samia kwa umma ili watu wamwelewe zaidi?

Kikatiba, Makamu wa Rais ni msaidizi wa Rais. Anatenda aliyopangiwa na Rais. Hata kuzungumza, anapaswa kutoa matamshi ambayo yanashabihiana na msimamo wa Rais. Je, msimamo wa Rais Samia kwa sasa ni Watanzania waamke na wapambane mpaka Katiba ipatikane?

Je, Nchimbi amechagua kuzungumza lugha za wanaharakati na wapinzani ili kujitengenezea mtaji binafsi kisiasa?

Haoni kwa kufanya hivyo anatikisa imani na hadhi ya Rais kwa umma? Yeye ndiye msaidizi wa Rais, kwa nini hamshauri Rais Samia njia bora na ya haraka ya kupata Katiba Mpya, badala yake anakimbilia kwa umma, kuchochea watu wakomae na wapambane? Na hayo mapambano ni dhidi ya nani? Je, ni dhidi ya Rais Samia ambaye naye anaitaka au kuna watu wanakwamisha? Nchimbi anazungumza kwa kuficha nukta.

Katika sanaa ya lugha na uwasilishaji, alichokifanya Nchimbi kinaitwa “Manipulative underspecification”, yaani unazungumza kwa namna ambayo unawaacha watu kila mmoja akijenga tafsiri na hitimisho lake.

Wakati huohuo, maana yako halisi unakuwa umeificha. Unafanya hivyo ili kumfanya kila mtu apende unachozungumza, wakati ukifahamu kwamba malengo yako ni tofauti.

Hata sasa, wapo wanaoamini kuwa Nchimbi anazungumza ili kujijenga kuelekea Uchaguzi 2030, anajisafishia njia ya urais. Wapo wanaomtetea.

Kimsingi, mtu akizungumza kwa mtindo wa “Manipulative Underspecification”, unakuwa huna namna ya kumpinga wala kumuunga mkono, maana anakuwa ameacha nafasi wazi. Hizo nafasi zilizo wazi ndizo zenye nukta ya Nchimbi. Ukiweza kuzijaza, basi utajua kwa usahihi kile anachomaanisha.

Схожие новости

#Наименование новостиТональностьИнформативностьДата публикации
1Masaju anavyoibua matarajio mhimili wa Mahakama01028-07-2026
2Minyukano Inavyozima ndoto za upinzani kushika dola01028-07-2026
3Kauli 'leo lazima niue mtu' ilivyogeuka hukumu ya kifo01029-07-2026
4Safari ya Kanali Kipingu kunoa kizazi cha wasomi nchini01028-07-2026
5Sendiga ‘anavyowateka’ wananchi kwa kujifananisha nao01028-07-2026
6Zanzibar inaandika ukurasa mpya au inarudia historia?01028-07-2026
7Lissu alivyowasili mahakamani kesi ya kikatiba01021-07-2026
8Mwalimu auawa akizuia mifugo kupita eneo la  shule06.0529-07-2026
9Tanzania: Power Infrastructure Vandalism Hits Muleba09.2629-07-2026
10Adaiwa kuuawa na mwenye changamoto ya akili akielekea msikitini07.9229-07-2026

Классификация: Информация. Схожих патентов: 0. Схожих новостей: 10. Тональность: 0. Информативность: 10. Источник: www.mwananchi.co.tz.